1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel na Iran zaendelea kushambuliana kwa siku ya 4

16 Juni 2025

Israel imefanya wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran siku ya Jumapili wakati Tehran nayo ikijibu kwa makombora mapya. Pande zote mbili zimetishia kufanya uharibifu zaidi katika mzozo ambao unaonekana kufukuta zaidi.

Israel Tel Aviv 2025 | Mfumo wa ulinzi wa anga wa Iron Dome wa Israel
Mfumo wa ulinzi wa anga wa Iron Dome wa Israel ukiingilia makombora ya IranPicha: Menahem Kahana/AFP

Mamlaka za Israel zimewaelekeza raia kuelekea kwenye maeneo salama ya kujikinga na mashambulizi, wakati Iran ikisema kuwa itaanza kufungua misikiti, vituo vya treni za metro na shule ili kutumika kama maeneo ya kujihifadhi, wakati Israel ikiendeleza mashambulizi. Vyombo vya habari vya Iran vyaripoti mlipuko mjini Tehran

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa Mkuu wa ujasusi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Mohammed Kazemi, ni miongoni mwa majenerali watatu waliuawa katika mashambuliziya Israel jana Jumapili.

Wizara ya afya ya Iran imeripotivifo vya watu 224tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi yake dhidi ya nchi hiyo mapema siku ya Ijumaa. Watu wengine zaidi ya 1,200 wamejeruhiwa, asilimia kubwa wakiwa ni raia.

Moto na moshi ukifuka katika anga ya Iran kufuatia shambulizi la IsraelPicha: Stringer/Getty Images

Kwa upande wa Israel, mamlaka zimeripoti vifo vya watu 13tangu Iran ilipochukua hatua ya kujibu mashambulizi.

Israel inasema mashambulizi yake yamepiga vituo vya kijeshi na nyuklia, na kuua maafisa wakuu na wanasayansi wa atomiki, lakini afisa mkuu wa Marekani alisema Jumapili kwamba Rais Donald Trump aliiambia Israel iachane na mpango wa kumuua kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei.

Wakati huo huo, maeneo ya makazi katika nchi zote mbili yameshambuliwa pakubwa tangu uhasama ulipozuka siku mbili zilizopita, huku waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiishutumu Iran kwa kuwalenga raia.

"Iran italipa gharama kubwa sana kwa mauaji ya kukusudia ya raia, wanawake na watoto," alisema Netanyahu wakati alipotembelea eneo la shambulio la kombora kwenye jengo la makazi katika mji wa pwani wa Bat Yam, karibu na Tel Aviv.

Milipuko mjini Tel AvivPicha: Leo Correa/AP Photo/picture alliance

Televisheni ya taifa ya Iran, wakati huo huo, iliripoti takriban watu watano waliouawa siku ya Jumapili katika shambulio la Israel lililopiga jengo la makazi katikati mwa jiji la Iran.Iran : Mashambulizi yatasitishwa Israel ikiacha uchokozi

Kanali Reza Sayyad, msemaji wa jeshi la Iran, alitishia "kuiadhibu vikali" Israel kwa mashambulizi. "Ondoka katika maeneo yanayokaliwa kwa sababu hayatakuwa tena makazi katika siku zijazo," alionya Kanali Reza katika hotuba yake kupitia televisheni, akiongeza kuwa makazi ya kujikinga na mabomu "hayatowahakikishia usalama".