1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Uingereza kupeleka walinzi wa amani 200 Kosovo

2 Oktoba 2023

Uingereza imetangaza kuongeza mchango wake katika kikosi cha ulinzi wa amani kinachoongozwa na Jumuiya ya Kujihami NATO nchini Kosovo.

Kosovo | Polizisten nach Schüssen in Banjska
Picha: OGNEN TEOFILOVSKI/REUTERS

Uingereza imetangaza hatua hiyo katika muda huu ambao kuna wasiwasi wa kukusanyika kwa wanajeshi wa Serbia kwenye eneo la mpaka.

Wizara ya Ulinzi ya taifa hilo imesema zaidi ya wanajeshi  200 watakwenda kuungana na wenzao 400 wa Uingereza ambao wapo Kosovo ikiwa kama sehemu ya mazoezi ya kijeshi ya  kila mwaka.

Kumekuwa na hali ya kuongezeka kwa mvutano ambapo Jumapili iliyopita, takribani wapiganaji 30 wa Serbia walikabiliana na polisi wa Kosovo katika kijiji cha Banjska huko Kaskazini mwa Kosovo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW