1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia ya safari za ndege na treni zafutwa Ujerumani

18 Januari 2024

Safari chungunzima za ndege za kuingia na kutoka viwanja mbali mbali vya ndege Ujerumani zafutwa.Takriban safari 500 za ndege zimefutwa uwanja wa Frankfurt kutokana na theluji na barafu.

Uwanja wa ndege wa Frankfurt-Ujerumani
Wasafiri wamekwama katika uwanja wa ndege wa FrankfurtPicha: Kirill Kudryavtsev/AFP

Hali ya hewa ya baridi kali na theluji pamoja na barafu imesababisha adha kubwa nchini Ujerumani na Ulaya kwa Ujumla wake. Usafiri wa barabarani,treni na ndege umetatizwa kwa siku ya pili leo (18.01.2024) kote Ujerumani.

Katika uwanja wa ndege wa Frankfurt, kituo kikubwa kabisa nchini Ujerumani cha safari za ndege zaidi ya safari  300 za kuingia na kutoka, kati ya takriban 1000 zilifutwa kwa mujibu wa msemaji wa uwanja huo.

Safari za treni kuelekea na kutoka Paris Ufaransa kwa mara nyingine nazo zilifutwa huku shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn likisema pamoja na kufutwa safari hizo bado safari nyingine za treni huenda zikafutwa kutokana na adha ya hali mbaya ya hewa. Katika uwanja wa ndege wa Munich hali pia haikuwa nzuri ambapo safari 250 kati ya 650 za ndege zilifutwa.  

Safari za ndege zimesitishwa katika uwanja wa Munich

Barabara kuu katika eneo la kati mwa Ujerumani zimeshuhudia msongamano mkubwa wa magari kwa mujibu wa polisi ambayo inasema usafishaji barabara zilizojaa theluji bado utachukuwa masaa mengi.

Katika jimbo la Baden-wuttenbern ajali nyingi za barabarani zimeripotiwa  karibu na eneo la baden baden ambapo inatajwa katika moja ya ajali dereva mwenye umri wa miaka 34 aligonga mti na kufa hapo hapo baada ya gari lake kuteleza na kuacha barabara.

Huduma ya Zima moto  na wanaotoa huduma ya kwanza katika jimbo la Rhineland Palatinate  walilazimika kuongeza nguvu zao kutowa huduma za dharura.

Madereva waombwa kujiepusha na safari zisizokuwa za lazima

Usafiri wa Treni katika mji wa Erfurt-UjerumaniPicha: Paul-Philipp Braun/IMAGO

Madereva wametakiwa kujiepusha na safari zisizokuwa za lazima katika kipindi hiki huku shule zikiwa zimefungwa kwa siku ya pili.

Vyombo vya habari vya ndani ,vimeripoti kwamba Jana usiku madereva walinasa katika milolongo mirefu ya magari katika barabara za Ujerumani ya Kati, na kulazimika kubakia katika msongamano kwa masaa chungunzima huku shirika la msalaba mwekundu likitowa  vinjwaji vya moto na mablanketi ya kujifunika kwa waliojikuta kwenye kadhia hiyo.

Mamia wafa kwa baridi Urusi

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Ujerumani ilitowa tahadhari kwamba theluji zaidi inatarajiwa kuanguka katika ambapo imeelezwa kwamba baadhi ya maeneo ya Kusini mwa nchi yataathirika zaidi na hali hiyo ya hewa. 

Kwa ujumla eneo zima la Ulaya ya Kaskazini hivi sasa linakabiliana na hali mbaya ya hewa ya theluji na baridi kali,nchini Norway katika eneo la nchi za Scandinavia viwanja vya ndege vilifungwa mjini Oslo kwa masaa chungunzima.

Katika nchi jirani ya Sweden hali pia ni mbaya ikishuhudiwa  msongamano wa magari na katika barabara nyingi za nchi hiyo.

Ulaya yakumbwa na baridi isiyo ya kawaida

00:51

This browser does not support the video element.

ap,reuters,dpa

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW