1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali mbaya ya usalama viwanjani

12 Januari 2006

. Wakati imebakia miezi mitano tu kabla ya kuanza mashindano ya kombe la dunia katika kandanda nchini Ujerumani,uchunguzi uliofanywa na shirika la udhibiti Warentest“ umeonyesha kwamba hali ya usalama katika viwanja vingi vya mpira ni ya kutisha.

Uwanja wa mpira nchini Ujerumani
Uwanja wa mpira nchini UjerumaniPicha: dfb

Katika uchunguzi wake shirika hilo limegundua kwamba viwannja vinne vya mpira havitimizi viwango vya usalama.Hatahivyo waandilizi wa mashindano wamesema kwamba uchunguzi huo umetia chumvi.

Uchunguzi wa shirika hilo linalozingatia viwango vinavyokubalika katika biadha na huduma,umeonyesha kwamba viwanja ambavyo kidogo ni salama ni vya Munic,Hannover,Nurnberg na Kolon.

Viwanja vilivyopewa kadi nyekundu katika uchunguzi huo ni vya Frankfrurt,Stuttgart na Dortmund.

Uwanja wa mji wa Kaiserslautern ndio unaosemekana kuwamo katika hali mbaya ukifuatiwa na viwanja vya Leipizig na Berlin.

Uchunguzi uliofanywa ulikuwa juu ya kuona iwapo watu wanaweza kuokelewa kama maafa yanatokea.

Wataalamu wanazingatia hasa umuhimu wa kuweza kukabiliana na hali za mijadhabiko.

Bwana Hubertus Primus wa shirika hilo la uchunguzi amesema mawezekano ya kutokea hali za mijadhabiko ni madogo lakini hatahivyo yapasa kutulia maanani hayo yanayozungumziwa.

Amsema katika shindano kati ya Costa Rica na Ujerumani hakuna mawezekano ya kutokea hali ya wasiwasi. Lakini purukushani inaweza kutokea katika mchezo baina ya Uingereza na Uholanzi ikiwa hatua za tahadhari hazitachukuliwa.

Mijadhabiko inaweza kusababishwa na mambo mambo mbalimbali,

Kwa mfano taa zikizimika watu wanaweza kushtushwa na kuanza kukanyagana. Hatari ya kutokea kiherehere pia inaweza kusababishwa na vitu vinavyoweza kutupiwa viwanjani

.

Viwanja vya Berlin na Leipzig vina kasoro katika milango ya dharura.

Viwanja hivyo vimejengwa ama kufanyiwa ukarabati kwa fedha kutoka serikalini kwa ajili ya msahindano ya kombe la dunia.

Ndiyo sababu mwenyekiti wa kamati ya michezo bungeni,bwana Peter Danckert wa chama cha SPD anataka kujua kwa uhakika juu kasoro zilizogunduliwa na shirika la udhibiti Warentest katika uchunguzi wake.hasa kwa kuzingatia kiasi cha fedha kilichotumika Amesema .mtu anashangaa kuona kwamba hakuna uwanja wenye viwango vya kimataifa licha ya fedha nyingi zilizotumika.

Lakini wajumbe wa kamati ya maandalizi wamesema uchunguzi uliofanywa na shirika la udhibiti wa viwango unafaa ufanyiwe upembuzi zaidi.

Makamu mwenykiti wa kamati hiyo bwana Horst R.Schmidt ameeleza kwa kuwa

sasa hakuna sehemu ya kusimama kwa watazamaji kama jinsi iliyvokuwa miaka mitano ama kumi iliyopita hapatakuwa na hatari .

Hatahivyo mwakilishsi wa shiriki la udhibiti wa viwango bwana Hubertus Primis amesema pana haja ya kuinua hali ya usalama ya viwanja

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW