1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali nchini Burundi

Hamidou, Oumilkher29 Aprili 2008

Marais wa zamani wa Burundi wanawatolea mwito serikali na wanamgambo wa FNL warejee katika meza ya mazungumzo

Rais Pierre Nkurunziza wa burundiPicha: AP


Watu wasiopungua 14,wameuliwa jana,12 kati yao ni wanaamgambo wa FNL,kufuatia mapigano nje ya mji mkuu Bujumbura.Marais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoy na Domitien Ndayizeye wamezihimiza pande zinazohusika zirejee katika meza ya majadiliano.Zaidi anasimulia Oummilkheir.


Gavana wa mkoa wa Bujumbura vijijini,mapigano hayo yalikotokea,Zénon Ndaruvukanye amesema mbali na wanamgambo hao 11,raia wawili pia wamepoteza maisha yao.


Leo asubuhi kumegunduliwa bufuru la kichwa lililovishwa kikofia cha rangi ya kijani cha jeshi pamoja na sehemu za siri za bwana mmoja zilizotundikwa katika kumbusho la umoja wa taifa karibu na ikulu ya rais mjini Bujumbura.Kumegundua pia kikaratasi kilichoandikwa tunanukuu: jeshi linasema uwongo linapodai halikula hasara " kikaratasi hico kimetiwa saini na wanamgambo wa FNL.


"Hatujapungukiwa na mwanajeshi hata mmoja,waliouliwa jana ni ama waasi au raia" Tunalaani kitendo hicho cha kinyama" alisema hayao mnsemaji wa jeshi,luteni kanali Adolphe Manirakiza.


Kuripuka upya mapigano kati ya jeshi la Burundi na wanamgambo wa Pelipehutu FNL kunadhihirisha makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyotiwa saini mwaka 2006 yana walakin.Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya anaitwika jukumu kubwa zaidi serikali na wapatanishi la kuzuka upya uhasama.Rais huyo wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya anaendelea kusema:


O-Ton Buyoya

"Wapatanishi wanabidi kutafakari.Kama hali ya mambo ni hii,hatuwezi kusema juhudi za upatanishi zimefanikiwa.Nnahisi pia Pelipehutu wanabidi watambue,historia ina tupa mifano chungu nzima ya wanamgambo shupavu,wanaoendelea kupigana bila ya kutilia maanani maagizo wala juhudi za amani na hatimae wanajikuta wakijiangamiza wenyewe."


Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya,mwemzake Domitien Ndayizeye akizungumzia pia mashambulio yasiyokwisha anawatolea mwito serikali na wanaamgambo wa FNL wakubali kurejea katika meza ya majadiliano kuzungumzia masuala ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi.

Domitien Ndayizeye anaendelea kusema:


O-Ton Ndayizeye

"Nionavyo mie ,bora watu wazungumze,badala ya kupalilia uhasama na kuzidisha makali ya mvutano nchini.Kila upande unajua unataka nini.Ndio maana püelipehutu wanalazimika kusitisha mashambulio na akuanza wakati huo huo kujadiliana juu ya masuala ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi."


Hali imeripotiwa kua shuwari hii leo katika eneo la Bujumbura vijijini mapigano yalikotokea jana.


Wanamgambo wameanza hujuma zao tangu Aperil 17 iliyopita mjini Bujumbura na katika mikoa minne ya magharibi ya Burundi.Kwa mujibu wa serikali watu 63 wamepoteza maisha yao.Duru nyengine zinazungumzia juu ya idadi kubwa kuliko hiyo.


Makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyotiwa saini september mwaka 2006 kati ya FNL na serikali,yamekwama kwasababu wanamgambo wanadai yaafikiwe makubaliano ya kugawana madaraka ya kisiasa na kijeshi-madai yanayokataliwa moja kwa moja na serikali.


►◄

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW