Hali nchini Mashariki ya Kongo baada ya uchaguzi
6 Desemba 2011Matangazo
Wakati matokeo ya uchaguzi ya rais yakisubiriwa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ripoti kutoka Beni kwenye mkoa wa Kivu ya Kaskazini, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, zinasema kuwa mapigano yalitokea alfajiri ya leo baina ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa Maimai, huku pia hali ikizidi kuwa ya wasiwasi katika eneo hilo, wanajeshi wakisambazwa katika mitaa ya eneo hilo.
Mwandishi wetu wa Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, John Kanyunyu, ametutumia taarifa ifuatayo:
Insert: Ripoti ya John Kanyunyu
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman