Hali sasa ni tulivu nchini Guinea
30 Septemba 2009Matangazo
Viongozi wa upinzani wamekula kiapo kuendelea na maandamano ya kuupinga utawala wa kijeshi wa Kapteni Moussa Dadis Camara, baada ya watu 157 kuuawa pale wanajeshi walipofyatua risasi dhidi ya waandamanaji Jumatatu iliopita. Maandamano hayo yaliitishwa na wanasiasa wa upinzani kupinga mpango wa Kiongozi wa kijeshi kutaka kuwa mgombea katika uchaguzi ujao akiwa na lengo la kubakia madarakani, licha ya kusema wakati alipotwaa madaraka kuwa hakuwa na azma hiyo. Mohamed AbdulRahman amezungumza na Mwandishi Habari na mchambuzi wa masuala ya Afrika Jenerali Ulimwengu akiwa Dar es salaam, na kwanza alimuuliza matukio haya yanaashiria nini katika siasa za Guinea chini ya uongozi wa sasa .
Mtayarishaji: Mohamed Abdulrahman
Mhariri: Othman Miraji