1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya hatari yatangazwa Guinea

18 Novemba 2010

CONAKRY

Guinea imetangaza hali ya hatari, nchini humo, baada ya kuzuka kwa mapigano ya kikabila yaliyosababisha vifo vya watu saba.

Rais wa mpito Generali Sekouba Konate alitoa tangazo hilo jana jioni baada ya kutokea machafuko kufuatia uchaguzi wa rais nchini humo. Hali hiyo ya hatari ni pamoja na marufuku ya kutotoka nje usiku, hadi pale matokea kamili ya uchaguzi yatakapoidhinishwa na mahakama kuu nchini humo.

Katika baadhi ya miji, marufuku ya kutotoka nje imewekwa hata mchana, huku kukiwa na ripoti za watu kupora mali.

 Mapema wiki hii matokeo ya awali yalionyeshwa Alpha Konde kiongozi wa muda mrefu wa upinzani ameshinda kwa asilia mia 52.5 katika duru hiyo ya pili ya uchaguzi w rais.Waziri Mkuu wa zamani Cellou Dalain Diallo alipata asili mia 47.5 ya kura.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW