JangaMarekani
Hali ya hatari yatangazwa New York kufuatia mafuriko makubwa
30 Septemba 2023Matangazo
Barabara za chini ya ardhi, mitaa na barabara kuu za mji huo zimefurika huku kituo kimoja cha uwanja wa ndege wa LaGuardia kikifungwa.
Gavana wa jimbo hilo Kathy Hochul amesema mvua ya hadi sentimita 12.7 imenyesha usiku kucha katika baadhi ya maeneo huku ikitarajiwa kuendelea.
Bi Hochul amewahimiza watu kusalia majumbani na kamwe "kutojaribu kusafiri kwenye barabara zilizojaa maji."
Licha ya kutotangazwa vifo au majeruhi hadi sasa, baadhi ya wakaazi wameingiwa na hofu.
Hali ya hatari pia imetangazwa katika mji wa Hoboken, jimbo la New Jersey.