1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya uchaguzi Pwani ya Kenya

10 Agosti 2022

Hali ni shwari mjini Mombasa, pwani ya Kenya huku shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea vizuri katika vituo tafauti vya kuhesabia kura nchini.

Ballot boxes and voting materials at Nyali polling station in Mombasa
Picha: Halima Gongo/DW

Wakenya wanaendelea kusubiri matokeo kwa hamu popote walipo huku bado kukiwa na hali ya wasiwasi wa kitakachojiri hasa kutokana na ghasia kuzuka hapo jana baada ya gavana wa Mombasa Hassan Joho na aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kuzozana katika kituo cha kupigia kura cha shule ya Msingi ya Marycliff eneo la Tudor,.

Zoezi la upigaji kura lilipokamilika, huku Mbunge wa Nyali Mohammed Ali akilazimika kukimbilia usalama wake ndani ya kituo cha polisi cha Nyali ili kuepuka mashambulizi kutoka kwa vijana waliokuwa na silaha ambao anadai ni wa mpinzani wake, 

Kwenye kituo cha shule ya Alidina Visram katika eneo bunge la Mvita, kumekuwa na shughuli nyingi za kuweza kutafuta uongozi mpya wa Mvita na kaunti ya Mombasa, katika nyadhifa mbali mbali za useneta, ubunge, uwakilishi wa kike na wodi huku uchaguzi wa ugavana ulioahirishwa ukitarajiwa kufanyika 23rd August 2022.

Usalama umeweza kudumishwa hapa huku maafisa wa polisi wakishika doria katika kila sehemu kuhakikisha hali ni tulivu wakati zoezi la kuhesabu kura linaendelea hapa.

Huenda kufikia jioni ya leo  washindi na washindwa watajulikana iwapo maafisa wa IEBC wataweza kukamilisha kila kitu.

Soma zaidi:Wakazi wa Mombasa watekeleza haki yao kikatiba

Kumekuwa na idadi ndogo ya wapiga kura hapa Mombasa ukilinganisha na miaka ya nyuma na kulingana na baadhi ya wakenya ikidhaniwa kuwa hiyo imesababishwa na kuahirishwa kwa uchaguzi wa ugavana wa Mombasa, lakini si Mombasa pekee ambayo idadi ya wapiga kura ilipungua, bali kenya nzima kinyume na matarajio ya tume huru ya uchaguzi IEBC.

DW-Mombasa