1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Hali ya usalama inazidi kuwa mbaya Goma

12 Aprili 2024

Huko Kivu Kaskazini, zaidi ya watu wanane wameuawa kwa kupigwa risasi katika muda wa Siku mbili mjini Goma. Vyanzo vya ndani vinasema ni zaidi ya wiki moja wakaazi wa mji huo wanaishi katika hali ya khofu

DR Kongo | M23
Mwanachama wa kundi la waasi la M23Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Limekuwa jambo la kawaida kusikika milio ya risasi katika mji wa Goma ambako raia wameendelea kuishi  katika hali ya khofu tangu kushuhudiwe na ongezeko la ghasia kwenye mzunguko wa mji huu. Taarifa zinasema kuwa watu wanane waliuwawa kwa kupigwa risasi  katika muda wa siku mbili katika mwa mji huu, Baadhi  waliuliwa usiku na wengine walishambuliwa  mchana na makundi ya wetu wenye silaha licha ya ulinzi mkubwa kutoka kwa wanajeshi wa serikali wanaofanya doria kila kukicha.

Usalama mashariki mwa Kongo waazidi kuzorota huku kundi la waasi yakijiimarisha

Baaadhi ya raia wameamua kuanza kuondoka katika maeneo hatarishi na kuelekea sehemu zinazo dhaniwa kuwa ni tulivu katikati mwa mji huu wenye idadi ya watu zaidi ya milioni moja. Judith Feza, anahangaika sasa baada ya kuyakimbia makaazi yake kufuatia mashambulizi ya watu wenye silaha walioilenga kwa risasi nyumba yake na kusababisha uharibifu mkubwa.

Mauaji yanazidi kuongezeka

Wakazi wa Goma wana wasiwasi wa namna hali inayoendelea kuwa mbaya nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya KongoPicha: Arlette Bashizi/REUTERS

Wakati huohuo, watu wengine wanne waliuawa kwa kupigwa risasi  wiki hii na wanaume waliovalia sare za jeshi kwenye manispaa ya majengo ,ambako kulingana na mashahidi ni mwanajeshi wa serikali ya kongo iliyewafyaria risasi vijana hao . Hata hivyo polisi ilisambaza mitandaoni picha za watu waliokamatwa na kutuhumiwa kuhusika na visa hivyo vya uhalifu kwenye mji wa Goma, ambao kulingana na mamkala yakijeshi watasikilizwa na vyomba vya sheria na baadae kuchukuliwa hatua za haraka.

"Tunahuzunika saana na hali mbaya ya usalama hapa kivu kaskazini,kila siku siku ni mauwa hii ni dhirihirisho kwamba viongozi wameshindwa sababu hesabu ya vifo imeongezako, tunaomba rais mwenyewe aingiliye kati swala hilo. Kwetu sisi kama raia hatuombe pesa laikini tunahitaji amani, " alisema Mungu Akonkwa mtetezi wa haki zabinadamu mashariki ya kongo.

Walinda amani UN waanza kuondoka DR Kongo

Video inayosambaa  mitandaoni tangu asubuhi ya leo ijumaa, imeonesha  miili ya watu wawili wote wakiwa ni vijana walipigwa riasi kwenye eneo la kyeshero linajawa na watu wengi.hadi sasa jeshi la serikali halieleza wazi kuhusu ongezeko la mauaji katika  mji huu ambamo vijana wazelendo walio idhinishwa nayo serikali ya kongo kama jeshi la akiba,wamekuwa wakirandaranda kote mjini Goma.

Mwandishi: Benjamin Kasembe

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW