HALI YA USALAMA YAIMARISHWA
23 Desemba 2003Matangazo
NEW YORK: Hatua za kulinda usalama katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa zimeimarishwa,baada ya serikali mjini Washington kuonya kuwa kuna kitisho cha mashambulio ya kigaidi.Waziri wa ndani wa Marekani Tom Ridge siku ya jumapili alitangaza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufanywa shambulio la kigaidi.Na siku ya jumatatu Rais George W.Bush aliwaambia wananchi waendelee na mipango yao ya kusheherekea Krismasi na mwaka mpya,licha ya kuwepo ulinzi mkali wa usalama.
