1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Hali ya utulivu imeshuhudiwa Sudan

23 Mei 2023

Hali ya utulivu imeshuhudiwa hii leo kote nchini Sudan ikiwa ni siku ya pili ya utekelezwaji wa makubaliano ya usitishaji mapigano.

Sudan Khartum | Gepanzertes Fahrzeug der Sudanesischen Armee
Picha: AFP/Getty Images

Utulivu huo wa muda unaongeza matumaini ya kusitishwa kabisa vita licha ya mashuhuda kadhaa kuripoti kuwa milio ya risasi ilisikika katika mji mkuu Khartoum.

Soma pia; Sudan: Makabiliano yaripotiwa baada ya kuanza usitishwaji mapigano kwa wiki moja

Baada ya zaidi ya mwezi mmoja wa mapigano, pande mbili hasimu za jeshi zilikubaliana kusitisha mapigano kwa siku saba kuanzia jana jioni ili kuruhusu utoaji wa misaada ya kiutu. Mzozo huo ambao unatishia kuvuruga usalama wa eneo hilo, umepelekea zaidi ya watu 250,000 kukimbilia nchi jirani.

Soma pia; Mahasimu Sudan kusitisha vita kwa siku saba

Mazungumzo ya usitishaji mapigano kati ya vikosi vya Abdel Fattah al-Burhan na vile vya Mohamed Hamdan Daglo yalifanyika mjini Jeddah kwa usaidizi mkubwa wa Saudi Arabia na Marekani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW