1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya wahamiaji Ujerumani

Lillian Urio16 Septemba 2005

Tangu miezi minane iliyopita Ujerumani ina sheria mpya ya uhamiaji. Sheria hiyo ilipitishwa baada ya miaka mingi ya majadiliano na inazingatia kuimarisha usimamizi wa uahamiaji, kuwapa wahamiaji uwezo wa kujumuika katika jamii na haki na ulinzi zaidi kwa wakimbizi wa kisiasa na wa aina nyingine

Lakini je sheria hii kweli imetekelezwa na kumekuwa na mabadiliko? Suala hili lilijadiliwa jana na wataalam wa mambo na wanasiasa katika mdahalo uliodhaminiwa na shirika la Otto Benecke. Shirika hilo linafanya kazi ya kuwasaidia wahamiaji kujumuika Ujerumani.

Ingawa hivi sasa kampeni kali za uchaguzi mkuu zinaendelea Ujerumani, lakini suala la uhamiaji halijakuwa zito sana katika kampeni za wakati huu. Bwana Wolfgang Bosbach, mwenyekiti msaidizi wa ushirikiano wa vyama vya kisiasa vya CDU na CSU anaridhika na sheria hizo mpya.

“Mimi binafsi nafurahi kwamba kuna ushirikiano mkubwa katika bunge wa vyama vyenye mlengo wa kulia. Tungeandika sheria hizo wenyewe zingekuwa tofauti. Na wangeandika vyama vinavyotawala sasa hivi, pia zingefanania vingine. Hii ni kwa sababu inapobidi mkubaliane, kila upande unawakilishwa.”

Bwana Bosbach anakubaliana na mtazamo wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bwana Otto Schily. Mwishoni mwa mwezi uliopita Waziri Schily alisema sheria hiyo mpya inazingatia nafasi za kazi zitakazopatikana kwa wakati ujao, bila kuingilia kazi za sasa hivi.

Tayari wafanyakazi 700 wa kigeni, wenye ujuzi wa hali ya juu, wameshahamia Ujerumani tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Kama vyama vya CDU na CSU vitashinda uchaguzi basi vinataka kuwaruhusu wahamiaji wenye ujuzi wa hali ya juu tu kuingia Ujerumani.

Chama cha Kijani kinataka kuwaruhusu wahamiaji wengi nchini, lakini serikali iongezee kasi ya kuwasaidia kujumuika na jamii ya Ujerumani. Lakini chama tawala cha SPD na chama cha upinzani cha CDU vimekwepa suala hili katika kampeni zao za uchaguzi.

Wakati huo huo takwimu zinaonyesha kwamba wahamiaji 200,000 wanaoingia kila mwaka Ujerumani hawatatosha kujaza nafasi za kazi zitakazojitokeza katika miaka ijayo, hasa kazi zinazohitaji ujuzi wa hali ya juu.

Lakini kuna mwanasiasa moja ambaye anazungumzia suala hili la uhamiaji katika kampeni zake.

Bwana Günther Beckstein, Waziri wa Mambo ya Ndani wa jimbo la Bayern na wa chama cha upinzani cha CSU, jana aliliambia gazeti la Berliner kwamba anataka kuwalazimisha wahamiaji wa Ujerumani kujumuika katika jamii.

Akimaanisha itawabidi wahamiaji wachukue mafunzo juu ya jamii ya Kijeumani na jinsi ya kujumuika katika jamii hiyo, yakiwemo masomo ya lugha ya Kijerumani.

Bwana Beckstein alisema kwa atakaye kataa kushiriki katika mafunzo hayo, basi atapunguziwa msaada wake wa fedha kutoka serikalini, kwa wale waiso kuwa na kazi.

Lakini menzake kutoka ushirikiano wa vyama vyao, Bwana Bosbach wa chama cha CDU hakubaliani naye kikamilifu.

“Hivi sasa mtu anahudhuria mafunzo kama hayo kwa hiari yake mwenyewe. Lakini pia kuna uwezo wa kumlazimu mtu kisheria ili achukue mafunzo ya lugha na ya kujumuika katika jamii.”

Pamoja na sheria hizo mpya kupongezwa, lakini kuna wanazozikosoa.

Bi Cornelia Schmalz-Jacobsen, aliyekuwa mwakilishili wa wahamiaji serikalini anasema ingawa mafunzo hayo ya uhamiaji ni mazuri lakini bado kuna tatizo katika elimu duni wanayopewa watoto wa wahamiaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW