Hali yakutisha yarejea Bangkok
19 Mei 2010Matangazo
Kiongozi mmoja wa waandamanaji hao Nattawut Saikua amesema wanajiandaa kukabiliana harakati hizo za serikali.Milio ya risasi imeendelea kusikika kutoka katika eneo hilo.Hapo jana serikali ya Thailand ilikataa upatanishi uliyotangazwa na Baraza la Seneti la nchi hiyo.
Afisa mmoja wa serikali hiyo alisema kuwa serikali itakuwa tayari kwa mazungumzo iwapo waandamanaji hao wataondoka kutoka katika eneo hilo.
Kiasi ya watu 39 wamekwishauawa mpaka sasa tokea kuibuka kwa mapigano mitaani kati ya polisi na waandamanaji hao Alhamisi iliyopita.
Mwandishi:Aboubakary Liongo