1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya yamkosoa Zelenskiy

6 Machi 2026

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imemkosoa vikali Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kwa kumtishia Waziri Mkuu Viktor Orban.

Msemaji wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Olof Gill
Msemaji wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Olof GillPicha: European Union, 202X, licensed under CC BY 4.0

Kitisho hicho cha Zelenskiy alikitoa katika mzozowa mkopo wa Umoja wa Ulaya wa thamani ya yuro bilioni 90 kwa Ukraine, ambao unazuiwa na Hungary.

"Tuko wazi kabisa kama Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya kwamba lugha kama hii haikubaliki. Hakustahili kuwa na vitisho dhidi ya mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya," alisema msemaji wa halmashauri hiyo Ijumaa.

Msemaji huyo ameongeza kuwa kuzidi kwa majibizanokati ya pande zote mbili hakusaidii.

Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskiyPicha: Danylo Antoniuk/Avalon/Photoshot/picture alliance

Hungary inazuia mkopo kutokana na uharibifu wa bomba la Druzhba

Hapo Alhamis, Zelenskiy alimshambulia Orban.

"Tunataraji mtu mmoja katika Umoja wa Ulaya hatozizuia yuro bilioni 90 na wapiganaji wa Ukraine watapokea silaha, la sivyo, tutatoa anwani ya mtu huyu kwa watu wetu ili wampigie na wazungumze naye kwa lugha yao," alisema Zelenskiy baada ya mkutano wa serikali mjini Kyiv.

Zelenskiy alisisitiza kuwa nchi yake haina namna nyengine mbali na huo mkopo wa Umoja wa Ulaya.

Serikali ya Hungary huko Budapest ilisema matamshi ya Zelenskiy ni "hujuma."

Budapest inazuia kutolewa mkopo huo wa Umoja wa Ulaya kutokana na kusitishwa usafirishaji wa mafuta kupitia kwa bomba la Druzhba.

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor OrbanPicha: Attila Kisbenedek/AFP/Getty Images

Kulingana na vyanzo vya Ukraine, bomba hilo liliharibiwa na droni ya Urusimwishoni mwa mwezi Januari karibu na mji wa magharibi wa Ukraine wa Brody.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW