1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

EU yapendekeza vikwazo vipya dhidi ya Urusi

16 Novemba 2023

Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya imependekeza vikwazo vipya vya duru ya 12 vya Umoja huo dhidi ya Urusi kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine

Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen akihutubia kongamano Brussels mnamo Novemba 8, 2023
Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Yves Herman/REUTERS

Pendekezo hilo linajumuisha vikwazo dhidi ya watu 120 zaidi pamoja na taasisi kwa jukumu lao katika kuhujumu uhuru na uadilifu wa kimaeneo wa Ukraine. Pendekezo hilo pia linajumuisha vikwazo vipya vya kuagiza na kusafirisha bidhaa nchini Urusi, pamoja na hatua za kudumisha ukomo wa bei ya mafuta na kukabiliana na ukwepaji wa vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya.

Wanaopendekezwa kuwekwa chini ya vikwazo vipya

Wanaopendekezwa kuorodheshwa chini ya vikwazo hivyo vipya ni pamoja na maafisa kutoka jeshi la Urusi, sekta za ulinzi na teknolojia ya habari pamoja na  wadau muhimu wa kiuchumi.

Wawakilishi wa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wanatathmini pendekezo hilo la vikwazo vipya vinavyopaswa kutekelezwa ifikapo mwisho wa mwaka .

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW