1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas inatafuta kufikia usitishaji vita haraka iwezekanavyo

Sylvia Mwehozi
4 Januari 2025

Kundi la wanamgambo la Hamas limesema katika taarifa yake kwamba lingependa kufikia makubaliano ya kusitisha vita "haraka iwezekanavyo" ili kuhakikisha Wapalestina wanarejea kwenye makazi yao.

Mwonekano wa uharibifu kufuatia shambulio la Israeli kwenye Hospitali ya Kamal Adwan
Mwonekano wa uharibifu kufuatia shambulio la Israeli kwenye Hospitali ya Kamal AdwanPicha: Khalil Ramzi Alkahlut/Anadolu/picture alliance

Kundi la wanamgambo la Hamas limesema katika taarifa yake kwamba lingependa kufikia makubaliano ya kusitisha vita "haraka iwezekanavyo" ili kuhakikisha Wapalestina wanarejea kwenye makazi yao katika Ukanda wa Gaza.Vyanzo: Mkataba usitishaji wa vita Gaza unakaribia

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Hamas wamesema makubaliano ya siku za usoni ya kusitisha mapigano yanapaswa kutumika ili kukomesha uchokozi dhidi ya raia wake na kuhakikisha jeshi la Israel linajiondoa katika Ukanda wa Gaza.

Duru mpya ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja ya kusitisha mapigano na kurejea kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas ilianza tena mjini Doha, Qatar siku ya Ijumaa.

Wakati huo huo, watu wapatao 30 waliuawakatika mashambulizi ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza, siku ya Ijumaa. Shirika la habari la Kipalestina WAFA, limeripoti kuwa miongoni mwa waliouawa ni mwandishi habari, wanawake na watoto.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW