1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yatathmini pendekezo jipya la Israel la kusitisha vita

27 Aprili 2024

Kundi la wanamgambo la Hamas limesema siku ya Jumamosi kuwa linatathmini pendekezo la hivi punde la Israel kuhusu uwezekano wa kufikia makubaliano ya usitishwaji mapigano huko Gaza, na kwamba wanajiandaa kutoa jibu lao.

Mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza
Uharibifu uliotokana na mashambulizi ya Israel katika mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa RafahPicha: Shadi Tabatibi/REUTERS

Siku ya Ijumaa, serikali mjini Cairo iliwatuma mjini Tel -Aviv wajumbe wa ngazi ya juu katika dhamira ya kufufua mazungumzo yaliyokwama na ambayo yamekuwa yakisimamiwa na Marekani, Misri na Qatar.

Soma pia:Mazungumzo ya kujadili vita vya Gaza kufanyika Saudi Arabia     

Hayo yanajiri wakati usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Israel imefanya mashambulizi ya anga katika mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Rafah na maeneo mengine na kusababisha vifo vya karibu watu 15.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW