Hamas itatoa msimamo baada ya kujadili mpango wa amani
30 Septemba 2025
Kundi la Hamas limesema litaujadili mpango wa amani wa rais Donald Trump ndani ya kundi hilo lakini pia na makundi mengine ya Palestina kabla ya kutowa msimamo wao.
Mpango huo wa amani wa Marekani tayari umeshaungwa mkono na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Qatar imetangaza mazungumzo na wajumbe wa Hamas na Uturuki
Kadhalika Qatar imesema inajiandaa kukutana na wajumbe wa kundi la Hamas wanaohusika kwenye mazungumzo pamoja na Uturuki, leo Jumanne kuujadili mpango huo wa amani ya Gaza ulioatangazwa na rais Donald Trump.
Ujerumani ni miongoni mwa mataifa ya Ulaya yaliyotangaza kuunga mkono mpango huo wa Trump. Urusi pia imeukaribisha mpango huo, ikisema inataraji utafanikiwa na kutekelezwa. Miongoni mwa mapendekezo yaliyoko kwenye mpango huo ni pamoja na kundi la Hamas kutakiwa kujisalimisha na kuweka chini silaha.