1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas kumuachia huru mateka wa Israel

12 Mei 2025

Mateka pekee aliyebakia hai,raia wa Marekani na Israel ataachiwa huru Jumatatu

Mateka raia wa Israel na Marekani anayeshikiliwa na Hamas
Mateka raia wa Israel na Marekani anayeshikiliwa na HamasPicha: Maya Alleruzzo/AP Photo/picture alliance

Kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza limesema litamuachia huru leo, mateka wa mwisho ambaye yuko hai, raia wa Marekani na Israel anayeshikiliwa huko Gaza.

Kundi hilo lilitowa taarifa hiyo jana Jumapili, bila ya kutowa ufafanuzi zaidi kuhusu hatua hiyo, na kusisitiza kwamba litamuachia huru, Edan Alexander kama ishara ya nia njema kwa utawala wa rais Donald Trump.Soma pia:Mpango wa Marekani juu ya misaada ya kiutu Gaza wapingwa

Israel imesema maandalizi yameshafanywa ya kumpokea mateka huyo mchana wa leo Jumatatu, kwa mujibu wa vyombo vya habari.Soma pia: Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani atoa wito wa amani

Awali ofisi ya Waziri mkuu Benjamin Netanyahu  ilisema kwamba mpango huo wa kuachiliwa raia wake Alexander unatarajiwa, ingawa haikuweka wazi wakati gani tukio hilo litafanyika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW