Hamas na Fatah wakabiliana
1 Januari 2008GAZA CITY
Wapalestina kiasi cha saba wameuwawa katika mapigano yaliyozuka ukanda wa gaza kati ya wafuasi wa chama cha rais Mahmoud Abas cha Fatah na wanachama wa Hamas.Mapigano hayo yalizuka katika mkutano wa hadhara uliokuwa ukifanyika katika eneo la Khan Yunis baada ya kikosi cha usalama cha Hamas kujaribu kuwatawanya watu ambapo kundi la wanachama wa Fatah waliaanza kuwafyatulia risasi Hamas.
Mapigano hayo yamezuka wakati rais Abbas akitoa mwito wa kuwepo mshikamano na umoja kwa wapalestina baada ya kumalizika mwaka mzima wa umwagikaji wa damu.
Katika hotuba yake ya hapo jana rais Abbas alisema yuko tayari kufanya mazungumzo na kundi la Hamas ikiwa kundi hilo litamkabidhi mamlaka ya eneo la Gaza.Hata hivyo chama cha Hamas kimesema kinaweza kuwa tayari kufanya mazungumzo na Abbas lakini bila ya kupewa masharti.