1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas na Fatah wakaribia makubaliano ya mtawala wa Gaza

4 Desemba 2024

Maafisa wa Palestina wamesema wawakilishi wa Fatah na Hamas wanakaribia kuhitimisha makubaliano ya kuteua kamati huru ya kisiasa ya wasomi, itakayosimamia Ukanda wa Gaza baada ya vita.

Gazastreifen Khan Yunis 2024 | Überschwemmte Zelte vertriebener Palästinenser
Wapalestina wakitathmini uharibifu wa mahema yanayotumiwa na watu waliokimbia makazi yao, kufuatia kuongezeka kwa kina cha bahari na mvua kubwa, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas, huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 25, 2024.Picha: Hatem Khaled/REUTERS

Afisa mmoja wa Mamlaka ya Palestina amethibitisha kwamba makubaliano ya awali yamefikiwa baada ya wiki kadhaa za mazungumzo mjini Cairo. Amesema kamati hiyo inaweza kuwa na wajumbe 12 hadi15, wengi wao kutoka Gaza.Kamati hiyo huenda ikauhitimisha utawala wa Hamas na pengine kusaidia kuendeleza mazungumzo ya kusitisha mapigano na Israel. Pande hizo hasimu zimefanya majaribio kadhaa ya upatanisho ambayo hata hivyo hayakuzaa matunda, tangu Hamas ilipochukua mamlaka huko Gaza mwaka 2007. Israel hata hivyo imeondoa uwezekano wa makundi hayo mawili kuitawala Palestina, inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW