1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas na Fatah watia saini makubaliano ya umoja, Beijing

23 Julai 2024

Makundi ya Kipalestina ya Hamas na Fatah yamesaini azimio la Beijing juu ya kumaliza mpasuko wa miaka mingi baina yao. Taarifa hiyo imetolewa na televisheni ya umma ya China CCTV, leo pasipo ufafanuzi zaidi.

Mahmoud al-Aloul na  Wang Yi
Makundi ya Kipalestina ya Hamas na Fatah yamesaini azimio la Beijing la kumaliza mpasuko baina yaoPicha: Pedro Pardo/AFP/Getty Images

Chombo hicho kilieleza azmio hilo pia linaatilia mkazo kustawisha umoja wa Wapalestina. Hatua hiyo imefikwa katika kipindi ambacho Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken akisema kuna ishara ya usitishwaji mapigano kati ya Israeli na Hamas.

Makundi hayo mawili hasimu ya Kipalestina, pamoja na mengine 12 ya kisiasa, walikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, kuhitimisha mazungumzo hayo yalianza Jumapili.

Hamas na Mamlaka ya Palestina wamekuwa na duru nyingi za mazungumzo ya umoja zilikuwa zinafeli tangu Hamas ilipovitimua vikosi vya Fatah kutoka Gaza katika unyakuzi mkali wa eneo hilo mwaka 2007.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW