1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas: Shambulizi la Israel kwenye shule limeua watu 100

10 Agosti 2024

Watu zaidi ya 100 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia shambulizi la Israel katika shule moja iliyokuwa ikiwahifadhi wakimbizi wa ndani katika Ukanda wa Gaza. Watu zaidi wanazidi kuangamia katika vita vya Gaza.

Gaza | Israel
Israel yashambulia shule iliyokuwa ikiwahifadhi wakimbizi katika Ukanda wa Gaza Picha: Omar Al-Qattaa/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa na utawala wa Hamas unaoongoza eneo hilo. Jeshi la Israel lilidai kuwa lililenga kituo cha kamandi cha wanamgambo hao wa Kipalestina.

Jeshi la Israel lashambulia shule Gaza na kuwaua watu 18

Wizara ya mambo ya nje ya Misri ililaani shambulizi hilo na kusema mauaji ya raia wa Gaza yanaonyesha kuwa Israel haikuwa na nia ya kusitisha vita. 

Misri, Marekani na Qatar wamepanga duru mpya ya mazungumzo ya kusitisha mapigano siku Alhamisi, wakati hofu ikiongezeka ya kutokea mzozo mkubwa zaidi wa kikanda, utakaozihusisha Iran na Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW