1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Hamas yaihimiza Marekani kuishinikiza Israel kusitisha vita

10 Juni 2024

Afisa mkuu wa kundi la Hamas, Sami Abu Zuhri ameihimiza Marekani kuishinikiza Israel kusitisha vita vyake katika Ukanda wa Gaza kabla ya ziara ya Waziri wa Mambo Nje wa Marekani Antony Blinken.

Gazastreifen Rauch nach israelischem Luftangriff
Moshi ukifuka katika Ukanda wa Gaza baada ya Israel kufanya shambulizi la angani katikati ya mzozo unaoendelea baina ya taifa hilo na kundi la HamasPicha: Emad Abu Shawiesh/REUTERS

Abu Zuhri ameongeza kuwa Hamas iko tayari kukubaliana na mpango wowote utakaofanikisha kukomeshwa kwa vita.

Kauli hii inajiri wakati Blinken anatarajiwa kufanya ziara yake ya nane Mashariki ya Kati akianzia Misri kabla ya kuelekea Israel leo Jumatatu, ziara inayolenga kuhakikisha kwamba vita havitanuki hadi Lebanon.

Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Marekani anatarajiwa kukutana na Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri mjini Kairo na baadaye Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant mjini Tel Aviv.

Ziara hii ni ya kwanza ya Biden tangu Rais  Joe Biden kutangaza pendekezo la kusitisha mapigano mnamo Mei 31.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW