1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas imebadilishana orodha ya mateka na wafungwa na Israel

8 Oktoba 2025

Kundi la wanamgambo la Hamas limesema Jumatano kuwa limebadilishana na Israel orodha ya majina ya mateka na wafungwa wa Palestina watakaoachiwa, chini ya mpango wa kubadilishana wafungwa na mateka.

Wanaharakati katika boti iliyovamiwa na jeshi la Israel Bahari ya Mediterenia
Wanaharakati katika boti iliyovamiwa na jeshi la Israel Bahari ya MeditereniaPicha: Freedom Flotilla Coalition/Handout/Anadolu/picture alliance

Wanamgambo hao vile vile wamesema wana matumaini kuhusiana na mazungumzo ya kusitisha mapigano yanayoendelea huko Misri katika mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump kuvimaliza vita vya Gaza.

Kulingana na chanzo cha Kipalestina kilichoko karibu na mazungumzo, muda wa kutekelezwa kwa awamu ya kwanza ya mpango huo wa hatua 20 wa Rais Trump bado haujakubaliwa katika mazungumzo hayo yanayofanyika katika mji wa Sharm el-Sheikh.

Haya yanafanyika wakati ambapo jeshi la Israel limezuia msafarawa kundi la boti tisa unaopeleka msaada Gaza mapema leo katika Bahari ya Mediterenia.

Ripoti zinaarifu kuwa wanaharakati 145 wanaoripotiwa kuwa katika hali nzuri ya kiafya wamekamatwa na wanapelekwa katika ufukwe wa Israel kwa ajili ya kurudishwa makwao.

Haya yanafanyika baada ya wanaharakati wengine 450 akiwemo Gtreta Thunberg kuzuiwa kuingia Gaza wiki iliyopita kwa ajili ya kutoa misaada. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW