HAMBURG. Kesi ya ugaidi yaahirishwa
8 Agosti 2005Kesi ya ugaidi inayomkabili raia wa Moroco Mounir el Motassadeq imeakhirishwa tena kwenye mahakama mjini Hamburg.
Motassadeq anakabiliwa na tuhuma za kushiriki katika kikundi cha kigaidi na mauaji ya sept 11 nchini Marekani, iwapo atapatikana na hatia katika makosa 3000 yaliyofunguliwa dhidi yake huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani.
El Moutassadeq amekiri kwamba aliwafahamu vyema marubani waliohusika na mauaji ya kigaidi ya sept 11 Mohamed Atta, Marwan al Shehi na Ziad Jarrah lakini amekanusha kuwa alijuwa mipango yao ya mashambulio ya kigaidi ya sep 11 nchini Marekani.
Kabla ya mawakili kufunga upande wa mashtaka wakili wa walio athiriwa katika shambulio la sept 11 aliiomba mahakama ya Hamburg ichunguze iwapo mtuhumiwa alikuwa na uhusianio na mwanachama mmoja wa kundi la kigaidi la al Qaeda Christian Ganczarski.