HAMBURG: Ujerumani kusaidia kupiga vita Ukimwi Afrika
31 Machi 2007Matangazo
Serikali ya Ujerumani inatazamia kutoa Euro bilioni mbili kwa misaada ya maendeleo barani Afrika katika kipindi cha miaka minne ijayo.Hiyo ni kwa mujibu wa jarida la Kijerumani “Spiegel”. Ahadi hiyo inatazamiwa kutolewa na Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel katika mkutano wa kilele wa nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda G-8 utakaofanywa mwezi wa Juni.Inasemekana,pesa hizo zinatolewa kusaidia miradi inayohusika na elimu na kupiga vita Ukimwi.