1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamilton aapa kutetea taji lake

Sekione Kitojo
14 Novemba 2016

Dereva wa magari ya Mercedes Lewis Hamilton ameapa kwamba anataka kutetea ubingwa wake uliomashakani kunyakuliwa na Dereva mwenzake Nico Rosberg katika mbio za mwisho msimu huu huko Abu Dhabi.

Mexiko Formel 1 Siegerehrung
Bingwa mtetezi wa mbio za magari za Formula one Lewis Hamilton (katikati)Picha: Getty Images/AFP/Y. Cortez

Na  katika  mbio  za  magari  Lewis  Hamilton  amemunya Nico Rosberrg kwamba  anawinda  ubingwa  wake  wa  nne wa  dunia  baada  ya  ushindi  wake  jana  nchini  Brazil na kusema  kuwa  ulikuwa  ushindi  wa  kirahisi  sana   katika ushindi  mara  52  wa  mbio  za  magari.

Dereva  huyo  mwenye  umri  wa  miaka  31  mzaliwa  wa Uingereza  alishnda  Grand Prix  ya  Brazil  kwa  mara  ya kwanza  katika  majaribio 10  na  kukamilisha  ushindi  mara tatu  mfululizo  na  kuweka  matumaini  yake  hai  ya kutetea  taji  lake  hilo, na  kusema  anawania  kushika nafasi  ya  kwanza  katika  mbio  za  mwisho  msimu  huu mjini  Abu  Dhabi  hapo  Novemba  27.

 

Mwandishi:  Sekione  Kitojo

Mhariri: Yusuf  Samu