1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamilton ashinda Azerbaijan Grand Prix

30 Aprili 2018

Katika mashindano ya magari ya Formula One, bingwa wa dunia wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton alishinda mashindano ya ya Grand Prix ya Azerbaijan na kutwaa uongozi wa msiamamo wa ubingwa wa dunia

Formel 1 - Großer Preis von Aserbaidschan
Picha: Reuters/D. Mdzinarishvili

Muingereza huyo alitwaa ushindi baada ya tairi la dereva mwenzake wa Mercedes Valtteri Bottas kulipuka wakati akiwa uongozini wakati naye Sebastian Vettel akafunga breki wakati alipotaka kumpiku.

Dereva huyo wa Ferrari ambaye alianza mashindano ya jana akiwa katika nafasi ya kwanza alimaliza wa nne. ""ni mbio ambazo zilikuwa na hisia nyingi kusema kweli. Valtteri alifanya kazi nzuri sana leo na ndiye aliyestahili kushinda. Pia Sebastian Vettel alifanya kazi nzuri. Nadhani nilikuwa na bahari nzuri sana sana leo, na nahisi sio kawaida kuwa hapa jukwaani, lakini nauchukua ushindi huo. SIkukata tamaa, niliendelea kupambana lakini hazikuwa mbio nzuri kwangu"

Dereva wa Ferrari Kimi Raikkonen alipanda jukwaani katika nafasi ya pili mbele ya Sergio Perez wa timu ya Force India. Ushindi huo wa kwanza wa Hamilton msimu huu, baada ya Vettel kuibuka mshindi katika mikondo miwili ya kwanza na Daniel Ricciardo wa Red Bull kutamba nchini China wiki mbili zilizopita, unamuweka mbele ya Vettel na pengo la pointi nne.

Nadal atamba Barcelona Open

Nadal alishinda taji lake la 11 la Barcelona OpenPicha: Getty Images/Y. Coatsaliou

Na katika tennis, mchezaji anayeorodheshwa nambari moja ulimwenguni Rafael Nadal alishinda fainali ya mashindano ya Barcelona Open dhidi ya Mgiriki Stefanos Tsitsipas hapo jana, na kuweka rekodi ya kubeba kombe hilo kwa mara ya 11. Nadal alimpongeza mpinzani wake "jana na leo zilikuwa mechi zangu nzuri kabisa. nna furaha kwa ushindi huu bila shaka dhidi ya mpinzani kama Tsitsipas. Nadhani ana maisha mazuri sana ya siku za usoni lakini nadhani ilikuwa fainali nzuri. nna furaha sana kunyakua taji la 11 hapa maana nilikuwa na wakati mzuri sana wiki nzima na kushangiliwa vizuri hapa. Ahsanteni sana. Chipukizi Tsitsipas ana umri wa miaka 19

FIFA yawachagua marefa 13 wa VAR

Marefarii 13 wamechaguliwa na Shirikisho la Kandanda Duniani - FIFA kuwa waamuzi wasaidizi wa video katika dimba la Kombe la Dunia nchini Urusi. FIFA imesema kuwa marefarii hao 13 watahudumu tu kama Waamuzi wasaidizi wa Video katika tamasha hilo litakaloanza Julai 14 hadi Juni 15. 9 kati ya marefarii hao wanatoka Ulaya, ikiwa ni watatu kutoka Italia na wawili kutoka Ujerumani na Ureno. Wawili wanatokea Amerika Kusinina mmoja kutoka shirikisho la Kandanda la Asia.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW