1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANNOVER: Ajali ya treni ya kasi imeua watu 23

23 Septemba 2006

Nchini Ujerumani,idadi ya watu waliofariki katika ajali ya treni yenye mwendo wa kasi- Transrapid,imefikia 23.Kwa mujibu wa polisi watu 10 walijeruhiwa.Treni hiyo iligongana na bogi la kiufundi katika mwendo wa kilomita 200 kwa saa kwenye njia ya reli ya kufanya majaribio, kaskazini mwa Ujerumani.Siku ya Ijumaa,Kansela Angela Merkel wa Ujerumani,alitembelea eneo la ajali.Waziri wa uchukuzi wa Ujerumani,Wolfgang Tiefensee ameivunja ziara yake nchini Uchina,ambako alikuwa akifanya majadiliano ya kuirefusha njia ya reli ya Transrapid katika jiji la Shanghai.Treni hiyo inayofanya safari kati ya uwanja wa ndege na jiji la Shanghai ni treni pekee ya kibiashara ya mwendo wa kasi- Transrapid.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW