HANNOVER: Ujerumani na Russia zashirikiana zaidi
12 Aprili 2005Matangazo
Ujerumani na Russia zimetia saini mikataba mbali mbali ya kiuchumi kwenye maonyesho ya biashara ya mwaka huu mjini Hannover,kaskazini mwa Ujerumani. Mikataba hiyo ina thamani ya Euro bilioni kadhaa. Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani na Rais Vladimir Putin wa Russia wameusifu upanuzi wa ushirikiano wao wa kiuchumi.Putin na Schroeder wamesisitiza uhusiano wa kiuchumi unaozidi kukuwa kati ya Ujerumani na Russia.Viongozi hao wamesema wanatazamia pia kushirikiana katika sekta za elimu na utafiti.Schroeder amesema msingi wa ushirikiano huo sasa umeshawekwa na ametoa muito kwa sekta ya binafsi kusaidia ushirikiano huo.Katika Maonyesho ya Hannover,mwaka huu Russia,ndio dola "rafiki".