HANOI : Kimbunga Xangsane kinakaribia pwani ya Vietnam
30 Septemba 2006Matangazo
Nchini Vietnam,kiasi ya watu 200,000 wamehamishwa kutoka eneo la pwani sehemu za kati za nchi hiyo ili kujiepusha na kimbunga kinachokuja kutoka Ufilipino.Kimbunga kilichopewa jina “Xangsane” kimeua si chini ya watu 62 nchini Ufilipino na wengine 68 bado hawajulikani walipo.Hicho ni kimbunga kibaya kabisa kupata kutokea Ufilipino tangu mwongo mmoja na kimewaacha mamilioni ya wakazi bila ya umeme katika kisiwa kikuu cha Luzon kaskazini mwa nchi.Maafisa wamesema,kama watu wapatao 90,000 hawawezi kurejea majumbani mwao kwa sababu ya hofu kuwa mmomonyoko wa ardhi huenda ukangoa nyumba.
