Hanover. Maonyesho ya biashara yafunguliwa, wenye viwanda kuuza zaidi nje.
17 Aprili 2007Maonyesho ya biashara ya kila mwaka mjini Hanover yamefunguliwa rasmi huku sekta ya uhandishi wa mitambo nchini Ujerumani ikitarajia mwaka wa mafanikio kwa mauzo makubwa, hususan nje ya nchi hii.
Chama chake cha VDMA, kimesema kuwa mauzo ya nje ya mitambo kutoka Ujerumani mwaka jana ilifikia kiasi cha Euro bilioni 123, na ukuaji hivi sasa ukiwa takriban kwa asilimia nne kwa mwaka.
Akitembelea maonyesho hayo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuingizwa kwa electronik za digital ambazo hutumia nishati kidogo katika mashine, kama vile pamp na kompresa, kumesaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mwaka huu nchi mgeni rasmi katika maonyesho hayo ya Hanover ni Uturuki. Kuna vibanda 276 miongoni mwa waonyeshaji 6,400 kutoka mataifa 60 katika uwanja huo wa maonyesho.