HARARE: Amri kumpeleka Simon Mann Equitorial Guinea
10 Mei 2007Matangazo
Mahakama nchini Zimbabwe imetoa amri ya kumpeleka Muingereza Simon Mann nchini Equitorial Guinea kukabiliana na mashtaka ya kupanga njama ya kutaka kuipindua serikali ya nchi hiyo miaka mitatu iliyopita.Mann,ambae hapo zamani alikuwa afisa maalum wa kijeshi,alikamatwa pamoja na watu wengine 61 katika uwanja wa ndege wa Harare mwaka 2004.Watu hao walishtakiwa kuitumia Zimbabwe kama kituo cha kukusanya silaha walizotaka kutumia kuipindua serikali ya rais Teodoro Obiang wa Equitorial Guinea.Hapo mwanzoni,Simon Mann alipewa kifungo cha jela cha miaka 7 lakini baadae kifungo hicho kilipunguzwa.