HARARE: Chama cha rais Mugabe chajinykulia ushindi.
4 Aprili 2005Matangazo
Kundi la wachunguzi 13 wa uchaguzi wa umoja wa nchi za Afrika limetoa ripoti yake na kusema kuwa limeridhishwa na jinsi uchaguzi wa bunge ulivyofanyika nchini Zimbabwe.
Uchaguzi wa hivi majuzi ulimalizika kwa chama cha ZANU PF cha rais Robert Mugabe kuibuka mshindi kwa kupata viti 78 dhidi ya viti 41 vya chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe MDC kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai.
Upinzani umelalamika kuwa uchaguzi huo ulijawa na visa vya udanganyifu vile vile Marekani na jamii ya Ulaya imesema tangu mwanzo kuwa hazina imani na uchaguzi wa Zimbabwe.
Wachunguzi wa umoja wa nchi za Afrika umeutaka upinzani nchini Zimbabwe kuchukua hatua za kisheria iwapo haukuridhika na matokeo ya uchaguzi huo.