HARARE: MDC kutoshiriki katika uchaguzi Zimbabwe?
6 Novemba 2005Matangazo
Chama cha upinzani nchini Zimbabwe MDC kimesisitiza msimamo wake kwamba hakitashiriki katika uchaguzi wa bunge la juu utakaofanyika baadae mwezi huu.
Lakini wanachama kadhaa wa ngazi za juu wa chama hicho walisusia mkutano wa baraza la kitaifa la chama hicho uliofanyika mjini Harare na kusema kwamba haukuwa halali.
Baraza hilo limetoa mwito kwa wanachama wao waliojiandikisha kushiriki katika uchaguizi huo waondoe majina yao.
Kiongozi wa chama cha MDC bwana Morgan Tsvangirai amesema hakuna haja ya kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuwa serikali itafanya udanganyifu
Hatahivyo watu wengi mashuhuri katika chama hicho hawakubaliani na msimamo huo wa bwana Tsvangirai.
.