HARARE: Mfumuko wa bei wavunja rekodi Zimbabwe
18 Mei 2007Matangazo
Mfumuko wa bei nchini Zimbabwe umeongezeka tena katika mwezi wa April na kuweka rekodi mpya ya asilimia 3,700.Kuongezeka maradufu kwa bei za bidhaa katika mwezi uliopita,kutazidi kumshinikiza Rais Robert Mugabe.Wakosoaji wanasema,mfumuko huo wa bei unasababishwa na sera za kiuchumi za Mugabe zenye utata pamoja na usimamizi mbaya.Idadi ya watu wasio na ajira pia imepanda hadi asilimia 80 huku Mugabe akichukua hatua kali dhidi ya upinzani na kujaribu kupuuza ukosoaji wa magharibi kuhusika na serikali yake.Mugabe alieshika madaraka tangu uhuru wa Zimbabwe,analaumu vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi kwa hali hiyo mbaya ya uchumi nchini humo.