HARARE: Mugabe asema Zimbabwe itafanya uchaguzi huru.
25 Machi 2005Matangazo
Serikali ya Zimbabwe imeanza matayarisho ya kiusalama huku uchaguzi wa bunge wa nchi hiyo ukikaribia.
Rais Robert Mugabe amesema kuwa serikali yake inafanya kila juhudi ili kuwepo na uchaguzi huru na wa haki ambao unasubiriwa kwa hamu na jamii ya kimataifa.
Chama cha upinzani cha Zimbabwe MDC kinasema kuwa chama tawala cha ZANU FP kinatumia vibaya vyombo vya habari kujifanyia kampeni.
Uchunguzi unaonyesha kuwa visa vya vurugu za kisiasa nchini Zimbabwe vimepungua huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika Machi 31.