HARARE: Rais Mugabe amerekebisha Katiba
2 Novemba 2007Matangazo
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametia saini rekebisho la katiba.Kuambatana na rekebisho hilo, bunge limepewa mamlaka ya kumchagua mrithi wa Mugabe,iwapo atastaafu au atafariki kabla ya kumaliza awamu yake.Bunge linadhibitiwa na chama cha Mugabe cha ZANU-PF kwa hivyo yeye anaweza kumteua mrithi wake.
Sheria mpya iliyotiwa saini vile vile inaruhusu kuitisha uchaguzi wa bunge miaka miwili kabla ya wakati wake,ili uweze kufanywa wakati mmoja na uchaguzi wa rais.Uchaguzi huo umepangwa kufanywa mwezi wa Machi.Rais Mugabe alie na umri wa miaka 83,anangángánia madaraka tangu mwaka 1980 na amesema,atagombea tena uchaguzi ujao.