Harare: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amedokeza kwamba nchi yake...
29 Novemba 2003Matangazo
huenda ikajitayarisha kujitoa kwenye Jumuiya ya Madola, Commonwealth. Mwaka jana Zimbabwe ilisimamishwa uwanachama wake katika jumuiya hiyo ya nchi 54, ambazo nyingi ni koloni za zamani za Muengereza. Hayo yalitokea baada ya Robert Mugabe kudai ushindi katika uchaguzi ambapo upande wa upinzani na makundi ya waangalizi kutoka nchi za Magharibi walisema ulifanyika kwa njia za udanganyifu.
Akizungumza katika redio ya serekali, Rais Mugabe alisema ikiwa gharama ya kupata kuingizwa tena katika Jumuiya ya Commonwealth ni kupoteza heshima ya utawala wa Zimbabwe, basi utafikia wakati kwa nchi hiyo kujitoa. Rais huyo hajaalikwa katika mkutano ujao wa kilele wa Commonwealth huko Nigeria.