Harare. Serikali ya Zimbabwe yakishutumu kituo cha utangazaji cha Sky cha Uingereza kwa kuishutumu serikali kwa kuwanyima raia wanaoipinga serikali chakula.
28 Machi 2005Chama tawala nchini Zimbabwe kimekishutumu kituo cha televisheni cha Sky nchini Uingereza kwa kuripoti kuwa viongozi wa chama hicho wanawanyima chakula kwa makusudi raia wa nchi hiyo ambao wanaunga mkono vyama vya upinzani kabla ya uchaguzi mkuu hapo siku ya Alhamis.
Kituo hicho cha televisheni nchini Uingereza kimetangaza mahojiano na mkosoaji mkuu wa rais Mugabe, bishop wa Kikatoliki Pius Ncube wa Bulawayo, ambaye alidai kuwa watu ambao hawaungi mkono serikali wanakataliwa kuchukua chakula katika vituo vya kugawa chakula cha dharura katika jimbo la kusini magharibi la Matabele.
Bwana Nathan Shamuyarira katibu wa mambo ya habari katika chama tawala cha Zanu PF amenukuliwa na gazeti la serikali la Herald nchini Zimbabwe akisema kuwa,kituo hicho cha televesheni kilifanya mahojiano na Ncube katika kanisa lake mjini Bulawayo na kutoa madai hayo na aliwataka wananchi wa Zimbabwe kupambana na serikali yao.
Bwana Shamuyarira amesema kuwa serikali imegawa chakula zaidi cha msaada katika jimbo la Matabele, suala linalojitokeza kuwa eneo la mapambano katika uchaguzi wa bunge, kwasababu jimbo hilo limeathirika mno na ukame na kwamba serikali iko tayari kutoa taarifa za utoaji wa chakula cha misaada.