HARARE: Tsvangirai afikishwa mahakamani-
2 Desemba 2003Matangazo
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe, Bwana Morgan Tsvangirai, anatazamiwa kufikishwa mahakamani leo hii, akishtumiwa makosa ya usaliti.
Bwana Tsvangirahi anashutumiwa kuhusika na njama za mauwaji dhidi ya Rais Robert Mugabe, wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2002.
Mawakili wa mashtaka wanatumia ukanda wa video, uliorikodiwa kwa siri, ambapo kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzanini MDC, anaonekana akizungumza na jasusi wa zamani nchini Israel, mazungumzo ambayo yanaelezewa kua yalilenga mauwaji dhidi ya Rais Mugabe.
Bwana Morgan Tsvangirai anakabiliwa na hukumu ya kifo ikiwa atakutwa na hatia, lakini amekanusha mashtaka dhidi yake, akidai tuhuma dhidi yake ni kampeni ya kumukashifu, ya Rais Robert Mugabe na chama chake cha Zanu / PF.