HARARE: Uchaguzi wa Bunge Kuu la Zimbabwe
8 Oktoba 2005Matangazo
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametangaza Novemba 26 kama tarehe ya kufanywa uchaguzi wa kulichagua bunge kuu.Bunge hilo jipya la wajumbe 66 litakuwa na machifu 10 wa kijadi,wabunge 50 watakaopigiwa kura na wengine 6 watakaochaguliwa na Mugabe.Bunge hilo linaundwa kufuatia mageuzi ya katiba ambayo pia hawazuia wakulima wa kizungu kuchukua hatua za kisheria,kuipinga sera ya kutwaa ardhi na vile vile huwazuia wakosoaji wa serikali kusafiri nchi za ngámbo.Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe,MDC bado hakijapitisha uamuzi wake ikiwa kishiriki katika uchaguzi huo,ambao MDC husema ni pigo kwa demokrasia.