HARARE: Uchaguzi wapamba moto nchini Zimbabwe
31 Machi 2005Matangazo
Watu milioni tano wamejiandikisha kupiga kura za uchaguzi wa wabunge hii leo. Kwa mujibu wa waangalizi uchaguzi huo umegeuka kuwa mzozo wa vizazi ambapo rais Mugabe mwenye umri wa miaka 81 anaunga mkono wagombea walio na umri mkubwa dhidi ya upinzani wenye vijana.
Rais Mugabe amewataka wapiga kura kukipinga chama cha upinzani cha MDC ambacho amekitaja kuwa kibaraka cha waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair.
Hata hivyo chama cha Mugabe cha Zanu PF kinatarajiwa kushinda katika uchaguzi huo.
Tofauti na uchaguzi wa mwaka 2000 na 2002 uliogubikwa na mizozo uchaguzi wa mwaka huu umetajwa kufanyika katika mazingira ya amani ingawa Umoja wa Ulaya umeukosoa uchaguzi huo na kutaja kuwa usiohalali.