1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE : Umoja wa Mataifa kusaidia ujenzi wa nyumba

9 Julai 2005

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayechunguza kuteketezwa kwa mitaa ya mabanda nchini Zimbabwe amesema hapo jana kwamba ofisi ya shirika la Makaazi la Umoja wa Mataifa itawekwa nchini humo kusaidia kushughulikia tatizo la nyumba za kuishi kulikosababishwa na bomowa bomowa ya mitaa hiyo ya mabanda.

Kufuatia mkutano wake na Rais Robert Mugabe na kumalizika kwa ziara yake ya siku 12 nchini humo mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa Anna Tibaijuka amesema afisa huyo anachaguliwa mara moja kuhakikisha wanafanikisha upatikanaji wa nyumba za kuishi za kudumu.

Tibaijuka amesema wasi wasi alio nao hivi sasa ni jinsi ya kuutekeleza mpango huo wa ujenzi mpya kuwapatia nyumba wale walipotezewa makaazi yao.

Serikali ya Zimbabwe ilianza kubomowa nyumba za mitaa ya mabanda tarehe 19 May kwa kuzitekeza katika kile ilichokieleza kuwa kampeni ya kutokomeza uchafu na uhalifu.

Umoja wa Mataifa unakadiria watu 200,000 wameachwa bila ya makaazi kufuatia kampeni hiyo lakini upinzani nchini Zimbabwe umeshutumu uteketezaji wa mitaa hiyo ya mabanda kuwa ni kampeni ya ukandamizaji na kusema kwamba watu wanaofikia milioni moja na nusu wamepoteza nyumba zao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW