HARARE: Usalama wa chakula barani Afrika
4 Oktoba 2005
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ameitetea sera yake ya kutwaa ardhi kama ni njia ya kuwapatia wananchi chakula.Mugabe alitamka hayo mjini Harare,alipoufungua mkutano unaofadhiliwa na mashrika ya Umoja wa Mataifa,ukihusika na usalama wa chakula barani Afrika.Kiasi ya wajumbe 170 wanahudhuria mkutano wa siku nne,unaotazamia kutayarisha mradi kuhusu usalama wa chakula barani Afrika.Kwa mujibu wa Hartwig de Haen,Naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa,FAO,lengo ni kuboresha usalama wa chakula kinachotumiwa na Waafrika na pia kuwasaidia wakulima wanaosafirsha bidhaa nje kufuatilia vizuri zaidi,vile viwango vilivyokuwepo katika nchi ambako mazao husafirishwa.Inakadiriwa kuwa barani Afrika,kila mwaka magonjwa yanayotokana na chakula na maji husababisha kiasi ya vifo 700,000.