Harare. Waandishi wa Uingereza waachiwa huru na mahakama nchini Zimbabwe.
14 Aprili 2005Matangazo
Mahakama moja nchini Zimbabwe imewaacha huru waandishi habari wawili kutoka Uingereza leo, kwa kosa la kuripoti kuhusu uchaguzi wa nchi hiyo bila idhini ya serikali, lakini sasa watashitakiwa kwa kosa la kubaki nchini bila ya visa.
Hakimu Never Diza amesema kuwa waendesha mashtaka wa serikali wameshindwa kuthibitisha kuwa Toby Harnden, mwandishi wa gazeti la Sunday Telegraph, na mpiga picha wake Julian Simmonds walikuwa wanafanyakazi nchini humo kinyume na sheria.