1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Watu 200 wazuiliwa na polisi nchini Zimbabwe

28 Mei 2007

Polisi nchini Zimbabwe wanasema wanawazuilia watetezi zaidi ya 200 wa upinzani na maafisa waliokamatwa juzi Jumamosi.

Watu hao wanatuhumiwa kuhusika kwenye mashambulio ya mabomu ya petroli dhidi ya vituo vya polisi, maduka na baadhi ya wafuasi wa serikali, yaliyofanywa hivi majuzi nchini Zimbabwe.

Lakini chama kikuu cha upinzani nchini humo, Movement for Democratic Change, kinasema madai kwamba wafuasi wake walifanya kampeni ya fujo dhidi ya utawala wa miaka 27 wa rais Robert Mugabe yana lengo la kuidhinisha ukandamizaji kabla kufanyika uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW